23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
24 Jiepushe na kinywa cha ujeuri,
Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
25 Macho yako yatazame mbele,
Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
26 Ebr 12:13Ulisawazishe pito la mguu wako,
Na njia zako zote zithibitike;
27 Isa 1:16Usigeuke kwa kulia wala kwa kushoto;
Ondoa mguu wako maovuni.