Publicidade

Provérbios 5

3 Maana midomo ya malaya hudondosha asali,

Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;

4 Mhu 7:26;Ebr 4:12Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga;

Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili.

5 Ebr 13:4Miguu yake inateremkia mauti;

Hatua zake zinashikamana na kuzimu;

6 Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima;

Njia zake ni za kutangatanga wala hana habari.

7 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa,

Wala msiache maneno ya kinywa changu.

8 Itenge njia yako mbali naye,

Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.

9 Usije ukawapa wengine heshima yako,

Na wakatili miaka yako;

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-