16 Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA;
Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.
17 Zab 5:6;Mit 12:22;Hos 4:1,2;Yn 8:44;Mit 1:11;Isa 1:15Macho ya kiburi, ulimi wa uongo,
Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
18 Mwa 6:5;Isa 59:7;Rum 3:15Moyo uwazao mawazo mabaya;
Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;
19 Zab 27:12Shahidi wa uongo asemaye uongo;
Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.