Utukufu wa baadaye wa Sayuni
1 "Imba, ewe mwanamke tasa,
wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto;
paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha,
wewe ambaye kamwe hukupata uchungu;
kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi
kuliko wa mwanamke mwenye mume,"
asema Mwenyezi Mungu.
2 "Panua mahali pa hema lako,
tandaza mapazia ya hema lako uyaeneze mbali,
wala usiyazuie;
ongeza urefu wa kamba zako,
imarisha vigingi vyako.
11 "Ewe mji uliyeteswa, uliyepigwa kwa dhoruba
na usiyetulizwa,
nitakujenga kwa almasi,
nitaweka misingi yako
kwa yakuti samawi.
12 Nitafanya minara yako ya akiki,
malango yako kwa vito ving’aavyo,
nazo kuta zako zote za vito vya thamani.
13 Watoto wako wote watafundishwa na Mwenyezi Mungu,
nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu.