6 "Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua:
kufungua minyororo ya udhalimu,
na kufungua kamba za nira,
kuwaweka huru waliodhulumiwa,
na kuvunja kila nira?
7 Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaa
na kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi,
unapomwona aliye uchi, umvike,
wala si kumkimbia mtu wa mwili wako
na damu yako mwenyewe?
8 Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko
na uponyaji wako utatokea upesi;
ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako,
na utukufu wa Mwenyezi Mungu utakuwa mlinzi nyuma yako.
9 Ndipo utaita, naye Mwenyezi Mungu atajibu,
utalia kuomba msaada,
naye atasema: Mimi hapa.
"Ukiiondoa nira ya udhalimu,
na kunyoosha kidole na kuzungumza maovu,