6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? 7 Mt 25:34;Zab 112:9;Mit 22:9;Mhu 11:1,2;Dan 4:27;Lk 11:41;Mwa 29:14;Neh 5:5;Mt 15:5Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usikose kumsaidia mtu aliye jamaa yako. 8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na uponyaji wako utatokea punde; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde. 9 Ndipo utaita, na BWANA ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;
Isaya 58:6-9
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
6 "Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua:
kufungua minyororo ya udhalimu,
na kufungua kamba za nira,
kuwaweka huru waliodhulumiwa,
na kuvunja kila nira?
7 Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaa
na kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi,
unapomwona aliye uchi, umvike,
wala si kumkimbia mtu wa mwili wako
na damu yako mwenyewe?
8 Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko
na uponyaji wako utatokea upesi;
ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako,
na utukufu wa Mwenyezi Mungu utakuwa mlinzi nyuma yako.
9 Ndipo utaita, naye Mwenyezi Mungu atajibu,
utalia kuomba msaada,
naye atasema: Mimi hapa.
"Ukiiondoa nira ya udhalimu,
na kunyoosha kidole na kuzungumza maovu,
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
6 "Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua:
kufungua minyororo ya udhalimu,
na kufungua kamba za nira,
kuwaweka huru walioonewa,
na kuvunja kila nira?
7 Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaa
na kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi,
unapomwona aliye uchi, umvike,
wala si kumkimbia mtu wa nyama na damu yako mwenyewe?
8 Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko
na uponyaji wako utatokea upesi;
ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako,
na utukufu wa Bwana utakuwa mlinzi nyuma yako.
9 Ndipo utaita, naye Bwana atajibu,
utalia kuomba msaada,
naye atasema: Mimi hapa.
"Kama ukiiondoa nira ya udhalimu,
na kunyoosha kidole na kuzungumza maovu,
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.