1 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu,
"Mbingu ni kiti changu cha enzi,
nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.
Iko wapi nyumba mtakayoijenga kwa ajili yangu?
Mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?
2 Je, mkono wangu haukuumba vitu hivi vyote,
hivyo vikapata kuwepo?"
asema Mwenyezi Mungu.
"Mtu huyu ndiye ninayemthamini:
yeye ambaye ni mnyenyekevu
na mwenye roho yenye toba,
atetemekaye asikiapo neno langu.