10 Mwenyezi Mungu akasema na Ahazi tena, 11 "Mwombe Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ishara, iwe kwenye vina virefu sana, au kwenye vimo virefu sana."
12 Lakini Ahazi akasema, "Sitaomba; sitamjaribu Mwenyezi Mungu."
13 Ndipo Isaya akasema, "Sikia sasa, ewe nyumba ya Daudi! Je, haitoshi kujaribu uvumilivu wa wanadamu? Je, mtaujaribu uvumilivu wa Mungu wangu pia? 14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara: Bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, na ataitwa Imanueli7:14 maana yake Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.