Isaya ampa Ahazi ishara ya Imanueli
10 Tena BWANA akasema na Ahazi akinena, 11 Jitakie ishara ya BWANA, Mungu wako; itake katika mahali palipo chini sana, au katika mahali palipo juu sana. 12 Lakini Ahazi akasema, Sitaitaka, wala sitamjaribu BWANA. 13 Mt 1:23;Lk 1:35;Isa 9:6;1 Tim 3:16Naye akasema, Sikilizeni sasa, enyi nyumba ya Daudi; Je! Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia? 14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto wa kiume, naye atamwita jina lake Imanueli.