1 Rut 4:11;Mit 24:3,4 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake;
Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
2 Ayu 12:4 Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA;
Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau.
3 Mit 12:6 Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi,
Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi.
4 Zizi ni safi ambapo hapana ng’ombe;
Bali nguvu za ng’ombe zaleta faida nyingi.
5 Kut 20:16 Shahidi mwaminifu hatasema uongo;
Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo.
6 Mit 17:24 Mwenye dharau hutafuta hekima, asiipate;
Bali maarifa huwa mepesi kwa mwenye ufahamu.
7 Toka mbele ya uso wa mpumbavu,
Maana hutaona kwake midomo ya maarifa.
8 Lk 12:20;1 Kor 3:19 Akili za mwenye busara ni kujua njia yake;
Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.
9 Mit 1:22 Wapumbavu huidharau hatia;
Bali upo upendeleo kwa wenye haki.
10 Moyo huujua uchungu wa nafsi yake,
Wala mgeni haishiriki furaha yake.
11 Ayu 8:15;Mit 3:33 Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa;
Bali hema la mwenye haki litafanikiwa.
12 Mit 16:25;Rum 6:21 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,
Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
13 Mhu 2:2 Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni;
Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo.
14 Mit 12:14;2 Kor 1:12;Flp 4:7 Ageukaye moyoni hushiba njia zake mwenyewe;
Na mtu mwema ataridhika nafsini mwake.
15 Mjinga huamini kila neno;
Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo.
16 Mit 22:3 Mwenye hekima huhadhari, na kujitenga na uovu;
Bali mpumbavu hupuuza yote, na hajali.
17 Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga;
Na mtu mwenye hila mbaya huzirwa.
18 Wajinga hurithi upumbavu;
Bali wenye busara huvikwa taji la maarifa.
19 Wabaya huinama mbele ya wema,
Na wasio haki malangoni mwao wenye haki.
20 Mit 19:7 Maskini huchukiwa hata na jirani yake;
Bali tajiri ana marafiki wengi.
21 Zab 41:1 Amdharauye mwenzake afanya dhambi;
Bali amhurumiaye maskini ana heri.
22 Je! Hawakosi wawazao mabaya?
Bali fadhili na kweli zina wao wawazao mema.
23 Katika kila kazi mna faida;
Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.
24 Taji la wenye hekima ni mali zao;
Bali upumbavu wa wajinga ni upumbavu tu.
25 Shahidi wa kweli huponya nafsi za watu;
Bali atoaye uongo hudanganya.
26 Kumcha BWANA ni tumaini imara;
Watoto wake watakuwa na kimbilio.
27 Mit 13:14 Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima,
Ili kuepukana na tanzi za mauti.
28 Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake;
Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao.
29 Mit 15:18;Mt 11:29;1 Kor 13:4,5;Yak 1:19 Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi;
Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.
30 Ayu 5:2;Zab 112:10;Mdo 7:9;Rum 1:29;Yak 4:5 Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili;
Bali husuda ni ubovu wa mifupa.
31 Ayu 31:15,16;Mhu 5:8;Mit 17:5;22:2;Mt 25:40;1 Yoh 3:17 Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake;
Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu.
32 Ayu 13:15;Zab 23:4;2 Kor 1:9;2 Tim 4:18 Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake;
Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.
33 Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu;
Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika.
34 Haki huinua taifa;
Bali dhambi ni aibu ya watu wowote.
35 Mt 24:45-47 Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara;
Bali hasira yake itakuwa juu yake aletaye aibu.