5 Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau;
Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
6 2 The 2:10Usimwache, naye atakusitiri;
Umpende, naye atakulinda.
7 Mt 13:44;Lk 10:42Bora hekima, basi jipatie hekima;
Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
8 1 Sam 2:30;Dan 12:3Umtukuze, naye atakukuza;
Atakupatia heshima, ukimkumbatia.