1 1 Fal 4:32Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.
Utangulizi
2 Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; 3 Mit 2:1kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. 4 Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na tahadhari;