Publicidade

Sabedoria

Por Bíblia Online

A sabedoria é um dos temas mais ricos da Bíblia. O temor do Senhor é seu princípio, e buscá-la vale mais que ouro ou prata. Deus promete dar sabedoria generosamente a quem pedir com fé.

O princípio da sabedoria

O temor do Senhor é o início de toda sabedoria verdadeira. Quem reverencia a Deus aprende a viver com discernimento e prudência.

Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.

Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima;

Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.

Kumcha BWANA ni maonyo ya hekima;

Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima,

Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri,

Sifa zake zadumu milele.

Bali hekima itapatikana wapi?

Na mahali pa ufahamu ni wapi?

Mwanadamu hajui thamani yake,

Wala haionekani katika nchi ya walio hai.

Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu;

Na bahari yasema, Haiko kwangu.

Haipatikani kwa dhahabu,

Wala fedha haitapimwa iwe thamani yake.

Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri,

Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti samawi.

Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo;

Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi.

Havitatajwa fedhaluka wala bilauri;

Naam, kima cha hekima chapita marijani.

Yakuti ya rangi ya manjano ya Kushi haitasawazishwa nayo,

Wala haitatiwa kima kwa dhahabu safi.

Basi hekima yatoka wapi?

Na mahali pa ufahamu ni wapi?

Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai,

Na kusitirika na ndege wa angani.

Uharibifu na Mauti husema,

Tumesikia habari zake kwa masikio yetu.

Sabedoria como dom de Deus

A verdadeira sabedoria vem do alto. Deus a concede generosamente a quem pede com fé, sem lançar em rosto a fraqueza humana.

Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima;

Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;

Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima;

Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;

Naam, ukiita busara,

Na kupaza sauti yako upate ufahamu;

Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA,

Na kupata kumjua Mungu.

Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana umetujulisha neno lile la mfalme.

Danieli akajibu, akasema, Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake.

Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.

A sabedoria do alto

A sabedoria que vem de Deus é pura, pacífica, amável, cheia de misericórdia e de bons frutos. Ela se opõe à sabedoria terrena e mundana.

Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.

Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.

Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.

Aina mbili za hekima

Ni nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aoneshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.

Hekima ya kweli ya Mungu

Lakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;

bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulubiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wagiriki ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wagiriki, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.

Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.

Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.

ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo; ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.

Direção e discernimento

Deus guia os humildes na justiça e ensina seu caminho aos mansos. Ele promete dirigir nossos passos quando confiamos nele de todo o coração.

Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,

Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

Katika njia zako zote mkiri yeye,

Naye atayanyosha mapito yako.

Usiwe na hekima machoni pako;

Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.

Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea;

Nitakushauri, jicho langu likikutazama.

Wenye upole atawaongoza katika haki,

Wenye upole atawafundisha njia yake.

Ee BWANA, unijulishe njia zako,

Unifundishe mapito yako,

Uniongoze katika kweli yako,

Na kunifundisha.

Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu,

Nakungoja Wewe mchana kutwa.

Hatua za mtu mwema huimarishwa na BWANA,

Naye huipenda njia yake.

Uniwezeshe kusikia fadhili zako asubuhi,

Kwa maana nimekutumaini Wewe.

Unifundishe njia nitakayoiendea,

Kwa maana ninakuinulia nafsi yangu.

Unifundishe kuyatenda mapenzi yako,

Kwa maana ndiwe Mungu wangu;

Roho yako mwema aniongoze katika njia iliyo sawa,

Ee BWANA, uniponye kwa ajili ya jina lako,

Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni;

Ee BWANA, unifundishe njia yako,

Na kuniongoza katika njia iliyonyoka;

Kwa sababu yao wanaoniotea;

A Palavra como fonte de sabedoria

A Palavra de Deus é lâmpada para os pés e luz para o caminho. Meditar nas Escrituras nos dá entendimento superior ao dos mestres.

* * *

Neno lako ni taa ya miguu yangu,

Na mwanga wa njia yangu.

* * *

Neno lako ni taa ya miguu yangu,

Na mwanga wa njia yangu.

Unifumbue macho yangu niyatazame

Maajabu yatokayo katika sheria yako.

Kufafanuliwa kwa maneno yako kunatia nuru,

Na kumfahamisha mjinga.

Njia mbili

Heri mtu yule asiyekwenda

Katika shauri la wasio haki;

Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi;

Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,

Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda,

Na uamkapo yatazungumza nawe.

Sabedoria prática para o dia a dia

A sabedoria se aplica em cada decisão: nas finanças, nos relacionamentos, no trabalho e no uso do tempo. Vivamos como sábios, não como insensatos.

Basi angalieni sana jinsi mnavyoenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana nyakati hizi ni za uovu.

Basi angalieni sana jinsi mnavyoenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana nyakati hizi ni za uovu.

Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho,

Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho.

Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho,

Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho.

Apataye hekima hujipenda nafsi yake;

Ashikaye ufahamu atapata mema.

Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana;

Na kwa shauri la akili fanya vita.

Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita;

Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.

Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi;

Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.

Kiburi huleta mashindano tu;

Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.

Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake;

Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.

Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe;

Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.

Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu;

Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.

Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo;

Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.

Moyo wa mwenye busara hupata maarifa;

Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa.

Mpumbavu hapendezwi na ufahamu;

Ila moyo wake udhihirike tu.

Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima;

Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.

mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.

Nendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolezwa chumvi, ili mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.

Nendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolezwa chumvi, ili mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.

Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.

O valor da sabedoria

A sabedoria é mais preciosa que rubis. Quem a encontra, encontra a vida e alcança o favor do Senhor. Nada se compara a ela.

Utajiri wa kweli

Heri mtu yule aonaye hekima,

Na mtu yule apataye ufahamu.

Maana yeye anionaye mimi aona uzima,

Naye atapata kibali kwa BWANA.

Si afadhali kupata hekima kuliko dhahabu?

Naam, yafaa kuchagua ufahamu kuliko fedha.

Moyo wa mtu huifikiri njia yake;

Bali BWANA huziongoza hatua zake.

Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu;

Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.

Kwa maana ulinzi wa hekima ni kama ulinzi wa fedha na ubora wa maarifa ni kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.

Usiseme, Kwa nini siku za kale zilikuwa ni bora kuliko siku hizi?

Maana si kwa hekima unauliza hili.

Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.

Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.

A sabedoria e a soberania de Deus

Os caminhos de Deus são mais altos que os nossos. Sua sabedoria é insondável, eterna e infinitamente superior ao entendimento humano.

Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, ndivyo njia zangu zilivyo juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.

Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.

Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.

Kuaibishwa na kuthibitishwa kwa mtumishi

Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.

Kuungana na Misri ni bure

Ole wao wateremkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti BWANA! Lakini yeye naye ana akili, naye ataleta uovu, wala hatayatangua maneno yake; bali ataondoka juu ya nyumba yao watendao mabaya, na juu ya msaada wa hao watendao maovu.

Hayo nayo yatoka kwa BWANA wa majeshi, mwenye shauri la ajabu, apitaye wote kwa hekima yake.

Na Roho ya BWANA itakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA; na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;

Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.

Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki!

Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina.

Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako!

Kwa hekima umevifanya vyote pia.

Dunia imejaa viumbe wako.

Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu,

Akili zake hazina mpaka.

Utaniongoza kwa shauri lako,

Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.

Basi, utufundishe kuzihesabu siku zetu,

Tujipatie moyo wa hekima.

Kinywa chake mwenye haki hunena hekima,

Na ulimi wake husema hukumu.

Nawe ujifurahishe katika BWANA,

Naye atakutimizia haja za moyo wako.

BWANA, uniongoze kwa haki yako,

Kwa sababu yao wanaoniotea.

Uinyoshe njia yako mbele ya uso wangu,

Utanijulisha njia ya uzima;

Mbele za uso wako kuna furaha tele;

Na katika mkono wako wa kulia

Mna mema ya milele.

Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawapitisha kwenye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.

Ee BWANA, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.

Ameiumba dunia kwa uweza wake,

Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake,

Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.

Usijisifu kwa ajili ya kesho;

Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja.

Watu waovu hawaelewi na haki;

Bali wamtafutao BWANA huelewa na zote.

Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.

Maonyo zaidi

Hii ndiyo mara yangu ya tatu kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.

tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana,

Mwanangu, usiyadharau maonyo ya Bwana,

Wala usife moyo ukiadhibiwa naye;

Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humuonya

Naye humpiga kila mwana amkubaliye.

Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.

Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Maovu ya siku yanaitosha siku hiyo.

Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.

Wasikiao na watendao

Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.

Basi msihukumu kwa kuangalia kwa nje tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.

Hekima ya Mungu katika uumbaji

Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi;

Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;

Wazee ndio walio na hekima,

Na katika kuishi siku nyingi iko fahamu.

Hekima na amri zina yeye [Mungu];

Yeye anayo ushauri na fahamu.

Ayubu ajibu: Hakuna mpatanishi

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

Kweli najua kuwa ndivyo hivyo;

Lakini mtu huwaje mwenye haki mbele za Mungu?

Kama akipenda kushindana naye,

Hawezi kumjibu neno moja katika elfu.

Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu;

Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?

Ee mwanadamu, yeye amekuonesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!

akawaambia hao waamuzi, Angalieni myafanyayo; kwa kuwa hammfanyii mwanadamu hukumu, ila BWANA; naye yupo pamoja nanyi katika neno la hukumu.

lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-04_21-26-40-