1 Haleluya.
Msifuni Bwana;
Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu sifa,
Maana ni mwenye fadhili, na anastahili kuimbiwa sifa.
2 Kum 30:3;Isa 27:13;Yer 32:37;Eze 36:24 BWANA ndiye aijengaye Yerusalemu,
Huwakusanya waliotawanyika wa Israeli.
3 Isa 61:1;Lk 4:18 Huwaponya waliopondeka moyo,
Na kuyaganga majeraha yao.
4 Mwa 15:5;Isa 40:26 Huihesabu idadi ya nyota,
Huzipa zote majina.
5 1 Nya 16:25;Nah 1:3 Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu,
Akili zake hazina mpaka.
6 Zab 146:8 BWANA huwategemeza wenye upole,
Huwaangusha chini wenye jeuri.
7 Efe 5:20 Mwimbieni BWANA kwa kushukuru,
Mwimbieni Mungu wetu kwa kinubi.
8 Ayu 38:20 Huzifunika mbingu kwa mawingu,
Huitengenezea nchi mvua,
Na kuichipusha nyasi milimani.
9 Ayu 38:41;Mt 6:26;Lk 12:24 Humpa mnyama chakula chake,
Wana-kunguru waliao.
10 Hos 1:7 Hapendezwi na nguvu za farasi,
Wala hairidhii miguu ya mkimbiaji.147:10 au mtu.
11 BWANA huwaridhia wao wamchao,
Na kuzitarajia fadhili zake.
12 Msifu BWANA, Ee Yerusalemu;
Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.
13 Maana amevikaza vipingo vya malango yako,
Amewabariki wanao ndani yako.
14 Ndiye aletaye amani mipakani mwako,
Hukushibisha kwa ngano safi.
15 Ayu 37:12 Huipeleka amri yake juu ya nchi,
Neno lake lapiga mbio sana.
16 Ndiye atoaye theluji kama sufu,
Huimwaga barafu yake kama majivu,
17 Hutupa mvua ya mawe kama makombo,
Mbele ya baridi yake ni nani awezaye kusimama?
18 Hulituma neno lake na kuviyeyusha,
Huuvumisha upepo wake, maji yakatiririka.
19 Kum 33:4;Mal 4:4;Rum 3:2 Hulitangaza neno lake kwa Yakobo,
Na amri zake na hukumu zake kwa Israeli.
20 Kum 4:32;Mdo 14:16;Rum 3:1-2 Hakulitendea taifa lolote mambo kama hayo,
Wala hukumu zake hawakuzijua.
Haleluya.