Publicidade

Salmos 25

Sala ya uongozi na ukombozi

Zaburi ya Daudi.

1 1 Sam 1:15;Zab 86:4;Omb 3:41 Ee BWANA, nakuinulia nafsi yangu,

2 Zab 7:1;18:2;Rum 10:11 Ee Mungu wangu,

Nimekutumainia Wewe, nisiaibike,

Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.

3 Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja;

Wataaibika watendao uhaini bila sababu.

4 Kut 33:13;Zab 143:8;Mit 8:20 Ee BWANA, unijulishe njia zako,

Unifundishe mapito yako,

5 Uniongoze katika kweli yako,

Na kunifundisha.

Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu,

Nakungoja Wewe mchana kutwa.

6 Ee BWANA, kumbuka rehema zako na fadhili zako,

Maana zimekuwako tokea zamani.

7 Zab 51:1 Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu,

Wala maasi yangu.

Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako,

Ee BWANA kwa ajili ya wema wako.

8 BWANA yu mwema, mwenye adili,

Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.

9 Wenye upole atawaongoza katika haki,

Wenye upole atawafundisha njia yake.

10 Njia zote za BWANA ni fadhili na kweli,

Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.

11 Zab 31:3;79:9;Rum 5:20 Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako,

Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi.

12 Zab 37:23 Ni nani amchaye BWANA?

Atamfundisha katika njia anayoichagua.

13 Zab 37:11,22,29 Watafanikiwa maishani mwao;

Na wazawa wao wataimiliki nchi.

14 Mit 3:32;Yn 7:17;2 Kor 4:2-6 Siri ya BWANA iko kwao wamchao,

Naye atawajulisha agano lake.

15 Zab 141:8 Macho yangu humwelekea BWANA daima,

Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.

16 Zab 69:16 Uniangalie na kunifadhili,

Maana mimi ni mkiwa na mteswa.

17 Uniondolee shida za moyo wangu,

Na kunitoa katika dhiki zangu.

18 2 Sam 16:12 Utazame mateso yangu na taabu yangu;

Unisamehe dhambi zangu zote.

19 Uwatazame adui zangu, maana ni wengi,

Na kwa namna wanavyonichukia kwa ukatili mwingi.

20 Unilinde nafsi yangu na kuniokoa,

Usiniache niaibike, maana nakukimbilia Wewe.

21 Ukamilifu na unyofu zinihifadhi,

Maana nakungoja Wewe.

22 Zab 130:8 Ee Mungu, umkomboe Israeli,

Katika taabu zake zote.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-04_23-13-58-