1 Yn 4:14;7:37;1 Kor 1:22;Mt 13:44;Ufu 21:6;3:18;22:17 Haya, kila aonaye kiu, njoni majini,
Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle;
Naam, njoni, nunueni divai na maziwa,
Bila fedha na bila gharama.
2 Kwa nini mtoe fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula?
Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha?
Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema,
Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.
3 Mt 11:28;Isa 54:8;2 Sam 7:8;Zab 89:28;Mdo 13:34 Tegeni masikio yenu, na kunijia;
Sikieni, na nafsi zenu zitaishi;
Nami nitafanya nanyi agano la milele,
Naam, rehema za Daudi zilizo imara.
4 Mal 3:5;1 Tim 6:13;Ufu 1:5;Eze 34:23;Dan 9:25;Ebr 2:10 Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa makabila ya watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa makabila ya watu. 5 Isa 52:15;Efe 2:11,12;Mdo 3:13 Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.
6 Zab 32:6;Amo 5:4,14;Mt 5:25;Yn 7:34;2 Kor 6:2;Ebr 3:13 Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana,
Mwiteni, maadamu yuko karibu;
7 Zek 8:17;Yer 3:12 Mtu mbaya na aache njia yake,
Na mtu asiye haki aache mawazo yake;
Na amrudie BWANA,
Naye atamrehemu;
Na arejee kwa Mungu wetu,
Naye atamsamehe kabisa.
8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. 9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, ndivyo njia zangu zilivyo juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. 10 2 Kor 9:10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; 11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
12 Maana mtatoka kwa furaha,
Mtaongozwa kwa amani;
Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo;
Na miti yote ya shambani itapiga makofi.
13 Badala ya michongoma utamea msonobari,
Na badala ya mibigili, mhadesi;
Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina,
Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.