Publicidade

Salmos 1

KITABU CHA KWANZA

Njia mbili

1 Mwa 5:24;Ayu 31:5;Zab 81:12;Mit 4:14 Heri mtu yule asiyekwenda

Katika shauri la wasio haki;

Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi;

Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

2 Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,

Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

3 Yer 17:8;Mwa 39:3;Zab 128:2 Naye atakuwa kama mti uliopandwa

Kandokando ya vijito vya maji,

Uzaao matunda yake kwa majira yake,

Wala jani lake halinyauki;

Na kila alitendalo litafanikiwa.

4 Sivyo walivyo wasio haki;

Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni,

Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.

6 Nah 1:7;Yn 10:14 Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki,

Bali njia ya wasio haki itapotea.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-04_23-13-58-