10 2 Kor 5:21;Gal 3:13;Rum 6:9;Efe 1:5Lakini BWANA aliridhika kumchubua;
Amemhuzunisha;
Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi,
Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi,
Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;
11 Yn 17:3;1 Yoh 2:1;Rum 5:18Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika.
Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki
Atawafanya wengi kuwa wenye haki;
Naye atayachukua maovu yao.
12 Flp 2:9;Kol 2:15;Mk 15:28;Lk 22:37;23:34Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu,
Naye atagawana nyara pamoja nao walio hodari;
Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa,
Akahesabiwa pamoja na hao wakosao.
Walakini alichukua dhambi za watu wengi,
Na kuwaombea wakosaji.