3 Zab 22:6;Ebr 4:15;Yn 1:10Alidharauliwa na kukataliwa na watu;
Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko;
Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,
Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
4 Mt 8:17;26:66;1 Pet 2:24Hakika ameyachukua masikitiko yetu,
Amejitwika huzuni zetu;
Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa,
Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5 1 Pet 2:24Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,
Alichubuliwa kwa maovu yetu;
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,
Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.