Publicidade

Isaías 55

Mwaliko wa maisha mema

1 Yn 4:14;7:37;1 Kor 1:22;Mt 13:44;Ufu 21:6;3:18;22:17Haya, kila aonaye kiu, njoni majini,

Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle;

Naam, njoni, nunueni divai na maziwa,

Bila fedha na bila gharama.

2 Kwa nini mtoe fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula?

Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha?

Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema,

Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.

3 Mt 11:28;Isa 54:8;2 Sam 7:8;Zab 89:28;Mdo 13:34Tegeni masikio yenu, na kunijia;

Sikieni, na nafsi zenu zitaishi;

Nami nitafanya nanyi agano la milele,

Naam, rehema za Daudi zilizo imara.

4 Mal 3:5;1 Tim 6:13;Ufu 1:5;Eze 34:23;Dan 9:25;Ebr 2:10Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa makabila ya watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa makabila ya watu. 5 Isa 52:15;Efe 2:11,12;Mdo 3:13Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.

6 Zab 32:6;Amo 5:4,14;Mt 5:25;Yn 7:34;2 Kor 6:2;Ebr 3:13Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana,

Mwiteni, maadamu yuko karibu;

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-