Publicidade

Isaías 61

Habari njema ya ukombozi

1 Mt 11:5;Lk 7:22;4:18;Isa 11:2;Yn 1:32;Zab 34:18;Hos 6:1;Zek 9:12;Yn 8:32-36 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2 Mt 5:4;Law 25:9;Mal 4:1-3 Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao; 3 Zab 30:11;Isa 60:21;Yn 15:8 kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe. 4 Eze 36:33 Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi. 5 Efe 2:12 Na wageni watasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabila nyingine watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu yenu. 6 Kut 19:6 Bali ninyi mtaitwa makuhani wa BWANA; watu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia utukufu wao. 7 2 Fal 2:9;Isa 40:2;Zek 9:12 Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele. 8 Isa 55:3 Maana mimi, BWANA, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wizi na uovu; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele. 9 Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika makabila ya watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na BWANA.

10 Ufu 21:2 Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu. 11 Zab 72:3;Isa 60:18 Maana kama nchi itoavyo machipuko yake, na kama bustani ioteshavyo vitu vilivyopandwa ndani yake; ndivyo Bwana MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele ya mataifa yote.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-