Pular para o conteúdo
Publicidade

Isaías 8

Mwana wa Isaya kuwa ishara ya uvamizi wa Ashuru

1 BWANA akaniambia, Ujipatie ubao mkubwa ukaandike juu yake kwa hati ya kawaida, Kwa Maher-shalal-hash-bazi;8:1 Kwa maana ya ‘kuteka kasi, kupokonya upesi’.2 2 Fal 16:10 nami nitajipatia mashahidi waaminifu ili kuandika habari, yaani, Uria, kuhani, na Zekaria, mwana wa Yeberekia. 3 Nami nikalala na nabii mwanamke, naye akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Kisha BWANA akaniambia, Mwite jina lake Maher-shalal-hash-bazi. 4 Isa 7:16 Kwa maana kabla mtoto huyo hajaweza kujua kusema, Baba yangu, na Mama yangu, hazina za Dameski na mateka ya Samaria yatachukuliwa mbele ya mfalme wa Ashuru.

5 Kisha BWANA akasema nami mara ya pili, akaniambia, 6 Neh 3:15;Yn 9:7 Kwa sababu watu hawa wameyakataa maji ya Shiloa yapitayo polepole, na kufurahi kwa ajili ya Resini na huyo mwana wa Remalia, 7 basi sasa angalia; Bwana aleta juu yao maji ya huo Mto, yenye nguvu, mengi sana, nayo ni mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote; naye atakuja, na kupita juu ya mifereji yake yote, atafurika juu ya kingo zake zote; 8 Isa 7:14;Mt 1:23 naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hadi shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.

9 Ungameni pamoja, enyi makabila ya watu,

Nanyi mtavunjwa vipande vipande;

Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali;

Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande;

Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande.

10 Ayu 5:12;Kum 20:1;Yos 1:5;Zab 46:7,11;Isa 9:6;Mt 1:23;Rum 8:31 Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika;

Semeni neno, lakini halitasimama;

Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.

11 Maana BWANA aliniambia hivi, kwa mkono hodari, akanifundisha nisiende katika njia ya watu hawa, akisema, 12 1 Pet 3:14-15 Msiseme, Ni njama, kuhusu mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni njama; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope. 13 Hes 20:12;Lk 12:5 BWANA wa majeshi ndiye mtakayemtakasa; na awe yeye hofu yenu, na awe yeye utisho wenu. 14 Eze 11:16;Lk 2:24;Rum 9:33;1 Pet 2:8 Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu. 15 Lk 20:18 Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa.

Wafuasi wa Isaya

16 Dan 12:4 Ufunge huo ushuhuda, ukaitie mhuri sheria kati ya wanafunzi wangu. 17 Hab 2:3;Lk 2:25;Ebr 2:13 Nami nitamngojea BWANA, awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia. 18 Zek 3:8;Ebr 2:13 Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa BWANA wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni.

19 Zab 106:28 Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? 20 Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi kulingana na neno hili, bila shaka kwa hao hakuna asubuhi. 21 Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu; 22 nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapatakuwa changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.

Veja também