Pular para o conteúdo
Publicidade

Isaya 11:6-9

SRUV Swahili Revised Union Version

6 Hos 2:18;Isa 65:25Mbwamwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwanasimba na ng’ombe wanono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. 7 Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe. 8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa kunyonya atatia mkono wake katika pango la fira. 9 Hab 2:14Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua BWANA, kama vile maji yanavyoifunika bahari.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    6 Mbwa-mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo,

    naye chui atalala pamoja na mbuzi,

    ndama, mwana simba na ng’ombe wa mwaka mmoja

    watakaa pamoja,

    naye mtoto mdogo atawaongoza.

    7 Ng’ombe na dubu watalisha pamoja,

    watoto wao watalala pamoja,

    na simba atakula majani makavu kama maksai.

    8 Mtoto mchanga atacheza karibu na shimo la nyoka,

    naye mtoto mdogo ataweka mkono wake

    kwenye kiota cha fira.

    9 Hawatadhuru wala kuharibu

    juu ya mlima wangu mtakatifu wote,

    kwa kuwa dunia itajawa na kumjua Mwenyezi Mungu

    kama maji yajazavyo bahari.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    6 Mbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo,

    naye chui atalala pamoja na mbuzi,

    ndama, mwana simba na ngʼombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja,

    naye mtoto mdogo atawaongoza.

    7 Ngʼombe na dubu watalisha pamoja,

    watoto wao watalala pamoja,

    na simba atakula majani makavu kama maksai.

    8 Mtoto mchanga atacheza karibu na shimo la nyoka,

    naye mtoto mdogo ataweka mkono wake

    kwenye kiota cha fira.

    9 Hawatadhuru wala kuharibu

    juu ya mlima wangu mtakatifu wote,

    kwa kuwa dunia itajawa na kumjua Bwana

    kama maji yajazavyo bahari.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.