Publicidade

Isaías 12

Shukrani na sifa

1 Isa 2:11;Zek 14:20,21 Na katika siku hiyo utasema,

Ee BWANA, nitakushukuru wewe;

Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia,

Hasira yako imegeukia mbali,

Nawe unanifariji moyo.

2 Kut 15:2;Zab 118:14 Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;

Nitatumaini wala sitaogopa;

Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu;

Naye amekuwa wokovu wangu.

3 Yer 2:13;Yn 4:10,14 Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu. 4 Na katika siku hiyo mtasema,

Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake;

Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa,

Litangazeni jina lake kuwa limetukuka.

5 Mwimbieni BWANA; kwa kuwa ametenda makuu;

Na yajulikane haya katika dunia yote.

6 Isa 54:1;Sef 3:14;Lk 19:37-40 Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;

Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-