12 Ufu 8:10;9:1Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni,
Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi!
Jinsi ulivyokatwa kabisa,
Ewe uliyewaangusha mataifa!
13 Omb 2:1;Dan 8:10;Ufu 12:4;Zab 48:2;Mt 11:23;Lk 10:15Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni,
Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu;
Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano,
Katika pande za mwisho za kaskazini.
14 Sef 2:15;2 The 2:4Nitapaa kupita vimo vya mawingu,
Nitafanana na yeye Aliye Juu.
15 Isa 47:8;Eze 28:8,9;Mt 11:23;Mdo 12:23Lakini utashushwa mpaka kuzimu;
Mpaka pande za mwisho za shimo.