Publicidade

Isaías 43

Ahadi ya matengenezo na ulinzi

1 Isa 44:6;42:6;1 Kor 1:9;2 Tim 1:9 Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. 2 Zab 66:12;Kum 31:6-8;Dan 3:25 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. 3 Mit 21:18 Maana mimi ni BWANA, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako. 4 Kut 19:5,6 Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na makabila ya watu kwa ajili ya maisha yako. 5 Isa 41:10,14;44:2 Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi; 6 nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia. 7 Isa 63:19;29:23;Zab 100:3;Yn 3:3;2 Kor 5:17;Efe 2:10 Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya. 8 Isa 6:9;42:19 Walete watu wasioona, japo wana macho, wasiosikia japo wana masikio. 9 Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli. 10 Yn 1:7;Mdo 1:8;Ebr 12:1;Ufu 1:5;Isa 44:8;41:8 Ninyi ni mashahidi wangu, asema BWANA, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. 11 Mimi, naam, mimi, ni BWANA, zaidi yangu mimi hapana mwokozi. 12 Kum 32:16 Nimetangaza habari, nimeokoa, nimeonesha, na hapakuwa mungu wa kigeni kati yenu; kwa sababu hiyo ninyi ni mashahidi wangu, asema BWANA, nami ni Mungu. 13 Zab 90:2;Mit 8:23;Mik 5:2;Mt 19:26 Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hakuna awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia?

14 BWANA, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Kwa ajili yenu nimetuma ujumbe Babeli nami nitawashusha wote mfano wa wakimbizi, naam, Wakaldayo, katika merikebu zao walizozifurahia. 15 Hos 13:10 Mimi ni BWANA, Mtakatifu wenu, Muumba wa Israeli, mfalme wenu. 16 Zab 77:19 BWANA asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu; 17 Kut 14:4 atoaye gari na farasi, jeshi la askari na uwezo; wamelala, hawataondoka; wametoweka, wamezimwa kama utambi. 18 Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. 19 2 Kor 5:17;Ufu 21:5 Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani. 20 Isa 48:21;Lk 1:74;Efe 1:5 Wanyama pori wataniheshimu, mbweha pia na mbuni; kwa sababu nimewapa maji jangwani, na mito nyikani, ili kuwanywesha watu wangu, wateule wangu; 21 watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu. 22 Mal 1:13 Lakini hukuniita, Ee Yakobo, bali umechoka nami, Ee Israeli. 23 Hukuniletea wana-kondoo kuwa kafara zako, wala hukuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukutumikisha kwa matoleo, wala sikukuchosha kwa ubani. 24 Isa 1:14;Mal 2:17;Yud 1:4 Hukuninunulia manukato kwa fedha, wala hukunishibisha kwa mafuta ya sadaka zako; bali umenitumikisha kwa dhambi zako, umenichosha kwa maovu yako. 25 Isa 44:22;Yer 31:34;Mik 7:18,19;Eze 36:22 Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. 26 Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. 27 Rum 5:12 Baba yako wa kwanza alifanya dhambi, na wakalimani wako wameniasi. 28 Isa 47:6;Omb 2:2;Zab 79:4;Yer 24:9;Dan 9:11;Zek 8:13 Kwa hiyo nitawatia unajisi wakuu wa patakatifu, nami nitamfanya Yakobo kuwalaani, na Israeli kuwa tukano.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-