Koreshi, chombo cha Mungu
1 Zab 73:23;Isa 41:13Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi45:1 Au, mtiwa mafuta (tazama 1 Sam 2:10). wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kulia, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza nguvu za wafalme;45:1 Katika Kiebrania ni: Nitalegeza viuno vya wafalme. ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. 2 Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukatakata mapingo ya chuma; 3 Kut 33:12nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.