Ibada aitakayo Mungu
1 1 Nya 28:2;2 Nya 6:18;Zab 11:4;Mdo 7:48,49;Mt 5:34-35;23:22BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani? 2 Zab 34:18;Ezr 9:4;Zab 119:120,161;Mit 28:14Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.