Utawala wa haki wa mfalme Ajaye
1 Mt 4:15;2 Fal 15:29;2 Nya 16:4;Law 26:24;1 Nya 5:26Lakini yeye aliyekuwa katika dhiki hatakosa changamko. Hapo awali aliiingiza nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali katika hali ya kudharauliwa, lakini zamani za mwisho ameifanya kuwa tukufu, karibu na njia ya bahari; ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa.
2 Isa 50:10;Yn 8:12;Efe 5:8;Mt 4:16;Lk 1:79Watu wale waliokwenda katika giza
Wameona nuru kuu;
Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti,
Nuru imewaangaza.
3 Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao;
Wanafurahi mbele zako,
Kama furaha ya wakati wa mavuno,
Kama watu wafurahivyo wagawanyapo nyara.
4 Amu 7:22;Zab 83:9;Isa 10:26Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake, na gongo la bega lake, na fimbo yake yeye aliyemwonea, kama katika siku ya Midiani. 5 Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyovingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni.
6 Lk 2:11;Yn 3:16;Mt 28:18;1 Kor 15:25;Amu 13:18;Zab 45:3,6;Yer 23:6;Yn 1:1;Tit 2:13;Efe 2:14;Kol 1:20;Ebr 13:20Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto wa kiume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,
Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.