Pular para o conteúdo
Publicidade

Jó 11

Sofari anena: Hatia ya Ayubu yastahili adhabu

1 Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu, na kusema,

2 Je! Huu wingi wa maneno usijibiwe?

Na mtu aliyejaa maneno, je! Ahesabiwe kuwa na haki?

3 Je! Majivuno yako yawanyamazishe watu wawe kimya?

Nawe hapo ufanyapo dhihaka, je! Hapana mtu atakayekutahayarisha?

4 Ayu 6:10;1 Pet 3:15 Kwa kuwa wewe wasema, Mafunzo yangu ni safi,

Nami ni safi machoni pako.

5 Lakini, laiti Mungu angenena,

Na kuifunua midomo yake juu yako;

6 Omb 3:22 Tena akuoneshe hizo siri za hekima,

Ya kuwa hufanikiwa katika kuyatimiza makusudi yake!

Ujue basi ya kuwa Mungu akuachilia katika uovu wako.

7 Ayu 5:9;Mhu 3:11;Isa 40:28;Mt 11:27;Rum 11:33;Efe 3:8 Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu?

Waweza kuufikia upeo wa huyo Mwenyezi?

8 Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe?

Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?

9 Cheo chake ni kirefu kuliko dunia,

Ni kipana zaidi ya bahari.

10 Yeye akipita, na kufunga watu,

Na kuwaita hukumuni, ni nani basi awezaye kumzuia?

11 Zab 10:11 Kwa kuwa yeye awajua watu baradhuli;

Anapouona uovu, je; hatauangalia?

12 Lakini mpumbavu aweza kupata ufahamu,

Ingawa mwanadamu huzaliwa kama mtoto wa punda mwitu.

13 1 Sam 7:3;Zab 78:8;143:6 Wewe ukiuweka moyo wako kwa uelekevu,

Na kumnyoshea mikono yako;

14 Ikiwa una uovu mkononi mwako, uweke mbali nawe,

Wala usikubali upuzi kukaa hemani mwako;

15 Mwa 4:5;Ayu 22:26;Zab 119:6;1 Tim 2:8;1 Yoh 3:21 Hakika ndipo utakapopata kuinua uso pasipo ila;

Naam, utathibitika, wala hutakuwa na hofu;

16 Kwa kuwa utasahau mateso yako;

Utayakumbuka kama maji yaliyokwisha pita;

17 Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri;

Giza lake litakuwa kama alfajiri.

18 Nawe utakuwa salama, kwa sababu kuna matumaini;

Naam, utatafutatafuta kando yako, na kupumzika salama.

19 Tena utalala, wala hapana atakayekutia hofu;

Naam, wengi watakutafuta uso wako.

20 Lakini macho ya waovu yataingia kiwi,

Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia,

Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.

Veja também