Bildadianena: Mungu huwaadhibu waovu
1 Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
2 Je! Hata lini utayawinda maneno kwa mitego?
Fikiri, kisha baadaye tutanena.
3 Ayu 12:7;Zab 73:22 Twahesabiwa kuwa wanyama kwa sababu gani,
Tena kuwa wanajisi machoni pako?
4 Ayu 13:14 Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako,
Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe?
Au jabali litaondolewa mahali pake?
5 Ayu 21:17;Mit 13:9 Naam, mwanga wa waovu utazimika,
Wala muali wa moto wake hautang’aa.
6 Mwanga hemani mwake utakuwa giza,
Nayo taa iliyo juu yake itazimwa.
7 Hatua zake za nguvu zitasongwa,
Na shauri lake mwenyewe litamwangusha chini.
8 Kwani ametupwa katika wavu na miguu yake mwenyewe,
Naye huenda juu ya matanzi.
9 Tanzi litamshika kisigino chake,
Na mtego utamshika.
10 Amefichiwa tanzi chini,
Na mtego amewekewa njiani.
11 Ayu 6:4;Zab 73:19;Yer 6:25;2 Kor 5:11 Vitisho vitamtia hofu kutoka kila upande,
Na kumfukuza karibu na visigino vyake.
12 Ayu 15:23;1 The 5:3 Nguvu zake zitaliwa na njaa,
Na msiba utakuwa tayari kwa kusita kwake.
13 Utakula via vya mwili wake,
Naam, mzaliwa wa kwanza wa mauti atavila via vyake.
14 Ayu 8:14;Zab 112:10;Mit 10:28;Mt 7:26,27 Atang’olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini;
Naye atapelekwa kwake mfalme wa vitisho.
15 Mwa 19:24 Katika hema yake hakuna kitakachobaki;
Kiberiti kitamwagwa juu ya makazi yake.
16 Chini, mizizi yake itakaushwa;
Na juu, tawi lake litasinyaa.
17 Zab 34:16;Mit 2:22 Kumbukumbu lake litakoma katika nchi,
Wala hatakuwa na jina mashambani.
18 Atakimbizwa kutoka mwangani hata gizani,
Na kufukuzwa atoke duniani.
19 Isa 14:22;Yer 22:30 Hatakuwa na mwana wala mjukuu kati ya watu wake,
Wala hatasalia mtu hapo alipokaa.
20 Hao wanaokaa magharibi watastaajabia siku yake,
Kama vile wanaokaa mashariki walivyotiwa hofu.
21 Yer 9:3;1 The 4:5;2 The 1:8;Tit 1:16 Hakika ndivyo yalivyo makazi ya wapotovu,
Na hapa ni mahali pake asiyemjua Mungu.