Pular para o conteúdo
Publicidade

Jó 25

Bildadi anena: Mtu awezaje kuwa mwenye haki mbele za Mungu

1 Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,

2 Enzi na hofu zi pamoja na Mungu;25:2 Katika Kiebrania ni naye.

Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.

3 Mwa 1:3-5,14-16;Zab 19:4-6;139:8,11;Mt 5:45;Yak 1:17 Je! Majeshi yake yahesabika?

Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?

4 Ayu 4:17;9:2;Zab 130:3;143:2;Rum 3:19,20 Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu?

Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?

5 Tazama, hata mwezi hauangazi,

Wala nyota si safi machoni pake;

6 Zab 22:6 Seuze mtu, aliye mdudu!

Na mwanadamu, ambaye ni buu!

Veja também