Ayubu ashikilia uelekevu wake
1 Kisha Ayubu akaendelea na hoja yake, na kusema,
2 Ayu 34:5 Kama aishivyo Mungu, aliyeniondolea haki yangu;
Huyo Mwenyezi aliyeitesa nafsi yangu;
3 (Kwa kuwa uhai wangu ungali mzima ndani yangu,
Na Roho ya Mungu iko katika pua yangu;)
4 Hakika midomo yangu haitanena yasiyo haki,
Wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
5 Ayu 13:15 Hasha! Nisiwahesabie ninyi kuwa na haki;
Hata nitakapokufa sitajiondolea uelekevu wangu.
6 Ayu 2:3;Mdo 24:16 Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha;
Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai.
7 Adui yangu na awe kama huyo mwovu,
Na mpinzani wangu awe kama asiye haki.
8 Mt 16:26 Maana tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida,
Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?
9 Mit 1:28;Isa 1:15;Mik 3:4;Zek 7:13;Yak 4:3 Je! Mungu atakisikia kilio chake,
Taabu zitakapomfikia?
10 Ayu 22:26 Je! Atajifurahisha katika Mwenyezi,
Na kumlingana Mungu nyakati zote?
11 Nitawafundisha ninyi mambo ya mkono wa Mungu;
Hayo yaliyo kwa Mwenyezi sitayaficha.
12 Tazama, ninyi nyote mmeyaona wenyewe;
Mbona basi mmebatilika kabisa?
13 Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kwa Mungu,
Na urithi wa hao waoneao, waupokeao kwa Mwenyezi.
14 Kum 28:32,41;Est 9:10;2 Fal 10:6-10 Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga;
Na wazao wake hawatashiba chakula.
15 Zab 78:64 Hao watakaosalia kwake watakufa kwa maradhi mabaya,
Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza.
16 Ajapokusanya fedha kama mavumbi,
Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa wingi;
17 Mit 28:8;Mhu 2:26 Yumkini kuyatengeza, lakini wenye haki watayavaa,
Nao wasio na hatia watazigawanya hizo fedha.
18 Omb 2:6 Yeye hujenga nyumba yake kama mdudu,
Na kama kibanda afanyacho mlinzi.
19 Hes 20:26 Yeye hujilaza hali ni tajiri, lakini ndio mwisho;
Hufunua macho yake, naye hayuko.
20 Vitisho vyampata kama maji mengi;
Dhoruba humwiba usiku.
21 Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka;
Na kumkumba atoke mahali pake.
22 Kwani Mungu atamtupia asimhurumie;
Angependa kuukimbia mkono wake.
23 Watu watampigia makofi,
Na kumzomea atoke mahali pake.