Pular para o conteúdo
Publicidade

Ayubu 38

4 Zab 104:5Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?

Haya! Sema, kama una ufahamu.

5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake hakika unajua!

Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?

6 Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?

Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,

7 Ayu 1:6Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,

Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?

8 Yer 5:22;Mwa 1:9;Zab 33:7;Mit 8:29Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango,

Hapo ilipotoka kwa nguvu kama kwamba imetoka tumboni mwa nchi.38:8 Katika Kiebrania hakuna mwa nchi.

9 Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake,

Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,

10 Nikaiagiza amri yangu;

Nikaiwekea makomeo na milango,

11 Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita,

Na hapa mawimbi yako yenye nguvu yatazuiliwa?

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também