Pular para o conteúdo
Publicidade

Ayubu 8

Bildadi anena: Ayubu astahili kutubu

1 Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema,

2 Wewe utanena maneno haya hadi lini?

Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hadi lini?

3 Mwa 18:25;Kum 32:4;Ayu 34:12;Dan 9:14 Je! Mungu hupotosha hukumu?

Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki?

4 Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi,

Naye amewatia mkononi mwa kosa lao;

5 Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii,

Na kumsihi huyo Mwenyezi;

6 Ikiwa wewe u safi na mwelekevu;

Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako,

Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.

7 Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo,

Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.

8 Kum 4:32 Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani,

Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta;

9 Mwa 47:9;Zab 39:5 (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno,

Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;)

10 Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza,

Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao?

11 Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope

Na makangaga kumea pasipo maji?

12 Zab 129:6;Yer 17:6;Yak 1:10,11;1 Pet 1:24 Yakiwa yangali mabichi bado, wala hayakukatwa,

Hunyauka mbele ya majani mengine.

13 Ayu 11:20;18:14;Zab 112:10;Mit 10:28;Isa 33:14;Mt 24:51;Lk 12:1,2 Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu;

Na matumaini yake huyo mbaya huangamia;

14 Uthabiti wake utavunjika,

Na matumaini yake huwa ni utando wa buibui.

15 Ayu 27:18 Ataitegemea nyumba yake, isisimame;

Atashikamana nayo, isidumu.

16 Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua,

Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake.

17 Mizizi yake huzongazonga chuguu,

Huangalia mahali penye mawe.

18 Ayu 7:10;Zab 37:36 Lakini, aking’olewa mahali pake,

Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona.

19 Zab 113:7 Tazama, furaha ya njia yake ni hii,

Na wengine watachipuka kutoka katika nchi.

20 Zab 37:24;1 The 5:23,24 Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu,

Wala hatawathibitisha watendao uovu.

21 Bado atakijaza kinywa chako kicheko,

Na midomo yako ataijaza shangwe.

22 Hao wakuchukiao watavikwa aibu;

Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também