Publicidade

Jó 13

1 Tazama, jicho langu limeyaona hayo yote,

Sikio langu limeyasikia na kuyaelewa.

2 Hayo myajuayo ninyi, na mimi pia nayajua;

Mimi si duni kuliko ninyi.

3 Hakika ningenena naye huyo Mwenyezi,

Nami nataka kuhojiana na Mungu.

4 Lakini ninyi hubuni maneno ya uongo,

Ninyi nyote ni matabibu wasiofaa.

5 Mit 17:28;Mhu 5:3;Amo 5:13;Yak 1:19 Laiti mngenyamaza kabisa!

Hilo lingekuwa hekima kwenu.

6 Sikieni sasa basi hoja zangu,

Mkayasikie malalamiko ya midomo yangu.

7 Ayu 17:5;Rum 3:5,8 Je! Mtanena yasiyo ya haki kwa ajili ya Mungu,

Na kusema kwa udanganyifu kwa ajili yake?

8 Mit 24:23 Je! Mtamwonesha yeye upendeleo?

Mtamtetea Mungu?

9 Je! Itafaa yeye kuwatafuta ninyi?

Au, kama kumdanganya mtu, je! Mtamdanganya yeye?

10 Hakika atawakemea ninyi,

Mkiwapendelea watu kwa siri.

11 Je! Huo ukuu wake hautawatia hofu,

Na utisho wake hautawaangukia?

12 Maneno yenu ya hekima ni mithali ya majivu,

Ngome zenu ni ngome za udongo.

13 Nyamazeni, niacheni, ili nipate kunena,

Na hayo yatakayonijia na yaje.

14 Zab 119:109 Nitaitwaa nyama ya mwili wangu katika meno yangu,

Na kuutwaa uhai wangu mkononi mwangu!

15 Zab 23:4;Mit 14:32;Rum 8:38,39;Ayu 27:5 Tazama, ataniua; sina tumaini;13:15 Au, ajaponiua, nitamngojea vivyo.

Ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake.

16 Isa 12:1,2 Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu;

Kwani asiyemcha Mungu hatakaribia mbele yake.

17 Sikieni sana maneno yangu,

Maelezo yangu na yaingie masikioni mwenu.

18 Angalieni sasa, nimekwisha kulitengeneza neno langu,

Najua ya kuwa mimi ni mwenye haki.

19 Ayu 33:6;Isa 50:8 Yuko nani atakayeshindana nami?

Maana sasa nitanyamaza kimya na kukata roho.

Ayubu atoa ombi la kukata tamaa

20 Lakini msinifanyie mambo mawili, hayo tu,

Ndipo nami sitajificha usoni pako;

21 Uondoe mkono wako usinilemee;

Na utisho wako usinitie hofu.

22 Basi uite wakati huo, nami nitaitika;

Au, niache ninene mimi, nawe unijibu.

23 Maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi?

Nijulishe kosa langu na dhambi yangu.

24 Zab 10:1;Isa 8:17;Omb 2:5;2 The 3:15 Mbona umeuficha uso wako,

Na kunihesabu kuwa ni adui yako?

25 Isa 17:13;42:3 Je! Utalitaabisha jani lipeperushwalo?

Au, je! Utayafuatia hayo mabua makavu?

26 Zab 25:7 Kwani umeandika maneno ya uchungu juu yangu,

Na kunirithisha maovu ya ujana wangu;

27 Ayu 33:11 Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyakagua mapito yangu yote;

Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu;

28 Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa,

Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-