Publicidade

Jó 26

Ayubu ajibu: Ukuu wa Mungu hauchunguziki

1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

2 Mit 25:11 Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo!

Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu!

3 1 Kor 2:4 Jinsi ulivyomshauri huyo asiye na hekima!

Na kutangaza ujuzi wa kweli kwa wingi!

4 Je! Umetamka maneno kwa nani?

Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?

5 Hao waliokufa watetemesha

Chini ya maji na hao wakaamo humo.

6 Zab 139:8;Mit 15:11;Isa 14:9;Amo 9:2;Ebr 4:13 Kaburi li wazi mbele yake,

Uharibifu nao hauna kifuniko.

7 Zab 24:1,2 Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu,

Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.

8 Mit 30:4 Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito;

Na hilo wingu halipasuki chini yake.

9 Husitiri uso wa kiti chake cha enzi,

Na kulitandaza wingu lake juu yake.

10 Yer 5:22 Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji,

Hata hapo mwanga na giza vinapopakana.

11 Nguzo za mbingu zatetemeka,

Na kustaajabu kwa kukemea kwake.

12 Kut 14:21;Isa 51:15;Zab 29:10;74:13 Huichafua bahari kwa uwezo wake,

Na kumtema Rahabu kwa akili zake.

13 Zab 33:6 Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake;

Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio.

14 Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake;

Na jinsi yalivyo madogo manong’ono tusikiayo katika habari zake!

Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuzielewa?

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-