20 Kum 9:18;Mt 26:39;1 Pet 5:6Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia; 21 Yak 1:17;Mwa 45:5;Amo 3:6;Efe 5:20akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nikiwa uchi, nami nitarudi tena huko uchi vile vile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.