4 Nao wanawe wa kiume huenda na kufanya karamu katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakawaalika dada zao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao. 5 Mwa 8:20;Ayu 42:8;2 Kor 11:2;1 Fal 21:10,13Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Pengine hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote.
18 Huyo alipokuwa angali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao wa kiume na wa kike walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa; 19 mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.