BWANA amjibu Ayubu
1 Kut 19:16,18;1 Fal 19:11;2 Fal 2:1;Eze 1:4Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,
2 Ni nani huyu atiaye ushauri giza
Kwa maneno yasiyo na maarifa?
3 Kut 23:13;1 Fal 18:46Basi jifunge viuno kama mwanamume,
Maana nitakuuliza neno, nawe niambie.
4 Zab 104:5Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?
Haya! Sema, kama una ufahamu.