4 Zab 104:5Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?
Haya! Sema, kama una ufahamu.
8 Yer 5:22;Mwa 1:9;Zab 33:7;Mit 8:29Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango,
Hapo ilipotoka kwa nguvu kama kwamba imetoka tumboni mwa nchi.38:8 Katika Kiebrania hakuna mwa nchi.
31 Ayu 9:9;Amo 5:8Je! Waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia,
Au kuvilegeza vifungo vya Orioni?
41 Zab 147:9;Mt 6:26;Lk 12:24Ni nani anayempatia kunguru chakula,
Makinda yake wanapomlilia Mungu,
Na kutangatanga kwa kutindikiwa na chakula?