Pular para o conteúdo
Publicidade

Jó 1

Ayubu na jamaa yake

1 Mwa 22:20;Yak 5:11;Mwa 6:9;Mit 8:13;1 Pet 3:11Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. 2 Kisha walizaliwa kwake watoto saba wa kiume, na binti watatu. 3 Mali yake nayo ilikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng’ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watumishi wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.

Veja também