1 Basi hao watu watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa sababu alikuwa mwenye haki machoni pake mwenyewe. 2 Mwa 22:21 Ndipo zikawaka hasira za huyo Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, katika jamaa ya Ramu, juu ya Ayubu, kwa sababu alikuwa amejipa haki mwenyewe zaidi ya Mungu. 3 Tena hasira zake ziliwaka juu ya hao rafiki zake watatu kwa sababu hawakupata jawabu, lakini wamemhukumia Ayubu makosa. 4 Basi huyo Elihu alikuwa anangoja ili anene na Ayubu, kwa sababu hao wengine walikuwa wazee kuliko yeye. 5 Hata Elihu alipoona kuwa hapana jawabu katika vinywa vya watu hao watatu, hasira zake ziliwaka.
6 Basi Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, akajibu, na kusema,
Mimi ni kijana, na ninyi ni wazee sana;
Kwa hiyo nilijizuia, nisithubutu kuwaonesha nionavyo.
7 Ayu 8:8,9 Nilisema, Yafaa siku ziseme,
Na wingi wa miaka ufundishe hekima.
8 1 Fal 3:9 Lakini hakika imo roho ndani ya mwanadamu,
Na pumzi ya Mwenyezi ndiyo impayo ufahamu.
9 1 Kor 1:21 Sio wakuu walio wenye hekima,
Wala sio wazee watambuao haki.
10 Basi nilisema, Nisikilizeni mimi;
Mimi nami nitawaonesha nionavyo.
11 Tazama, niliyangojea maneno yenu,
Nilizisikiliza nisikie hoja zenu,
Hapo mlipokitafuta mtakalonena.
12 Mit 18:13 Naam, niliwasikiza ninyi,
Na tazama, hapana mmoja aliyemshinda Ayubu,
Wala kumjibu maneno yake, kati yenu.
13 Yer 9:23 Jitunzeni msiseme, Sisi tumepata hekima;
Mungu huenda akamshinda, si mtu;
14 Kwa kuwa yeye hajayaelekeza maneno yake kwangu;
Wala sitamjibu mimi kwa maneno yenu.
15 Wameshangaa, hawajibu tena;
Hawana neno la kusema.
16 Na mimi, je! Ningoje, kwa sababu hawaneni,
Kwa sababu wasimama kimya, wala wasijibu tena;
17 Mimi nami nitajibu sehemu yangu,
Mimi nami nitaonesha nionavyo.
18 Kwa kuwa nimejaa maneno;
Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.
19 Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa;
Kama viriba vipya liko karibu kupasuka.
20 Nitanena, ili nipate kutulia;
Nitafunua midomo yangu na kujibu.
21 Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu;
Wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote.
22 Mdo 12:22,23 Kwa kuwa mimi sijui kujipendekeza;
Au Muumba wangu angeniondoa kwa upesi.