4 Zab 104:5Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?
Haya! Sema, kama una ufahamu.
5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake – hakika unajua!
Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?
8 Yer 5:22;Mwa 1:9;Zab 33:7;Mit 8:29Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango,
Hapo ilipotoka kwa nguvu kama kwamba imetoka tumboni mwa nchi.38:8 Katika Kiebrania hakuna mwa nchi.
12 Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza?
Umeyajulisha mapambazuko mahali pake?
31 Ayu 9:9;Amo 5:8Je! Waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia,
Au kuvilegeza vifungo vya Orioni?