1 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Vyote vilivyomo ndani yangu
vilihimidi jina lake takatifu.
2 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,
wala usisahau wema wake wote,
3 akusamehe dhambi zako zote,
akuponya magonjwa yako yote,
4 aukomboa uhai wako na kaburi,
akuvika taji ya upendo na huruma,