Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 128

Thawabu Ya Kumtii Bwana

Wimbo wa kwenda juu.

1 Heri ni wale wote wamchao Bwana,

waendao katika njia zake.

2 Utakula matunda ya kazi yako;

baraka na mafanikio vitakuwa vyako.

3 Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao

ndani ya nyumba yako;

wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni

kuizunguka meza yako.

4 Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa

mtu amchaye Bwana.

5 Bwana na akubariki kutoka Sayuni

siku zote za maisha yako,

na uone mafanikio ya Yerusalemu,

6 nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako.

Amani iwe juu ya Israeli.

Veja também