Maombi Ya Shukrani
1 Nitakutukuza wewe, Ee Bwana,
kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi,
na hukuacha adui zangu
washangilie juu yangu.
2 Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie
na wewe umeniponya.
3 Ee Bwana, umenitoa Kuzimu,
umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.