Kusifu Mungu Kwa Ajili Ya Wema Wake
1 Mpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote!
2 Imbeni utukufu wa jina lake;
mpeni sifa zake kwa utukufu!
3 Mwambieni Mungu, "Jinsi gani yalivyo ya kutisha matendo yako!
Uwezo wako ni mkuu mno kiasi kwamba
adui wananyenyekea mbele zako.
4 Dunia yote yakusujudia,
wanakuimbia wewe sifa,
wanaliimbia sifa jina lako."