1 Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu,
sikilizeni maneno ya kinywa changu.
2 Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo,
nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale:
3 yale ambayo tuliyasikia na kuyajua,
yale ambayo baba zetu walituambia.
4 Hatutayaficha kwa watoto wao;
tutakiambia kizazi kijacho
matendo yastahiliyo sifa ya Bwana,
uweza wake, na maajabu aliyoyafanya.