Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 139:1-18

Mwenyezi Mungu asiyeweza kukwepwa

1 Ee Mwenyezi Mungu, umenichunguza

na kunijua.

2 Unajua ninapoketi na ninapoinuka;

unatambua mawazo yangu tokea mbali.

3 Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu;

unaelewa njia zangu zote.

4 Kabla neno halijafika katika ulimi wangu,

wewe walijua kikamilifu, Ee Mwenyezi Mungu.

5 Umenizingira nyuma na mbele;

umeweka mkono wako juu yangu.

6 Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu,

ni ya juu sana kwangu kuyafikia.

7 Niende wapi nijiepushe na Roho yako?

Niende wapi niukimbie uso wako?

8 Nikienda juu mbinguni, wewe uko huko;

nikifanya vilindi139:8 Vilindi ina maana ya Kuzimu; kwa Kiebrania ni Sheol. kuwa kitanda changu,

wewe uko huko.

9 Nikipanda juu kwa mabawa ya mapambazuko,

nikikaa pande za mbali za bahari,

10 hata huko mkono wako utaniongoza,

mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti.

11 Nikisema, "Hakika giza litanificha

na nuru inayonizunguka iwe usiku,"

12 hata giza halitakuwa giza kwako,

usiku utang’aa kama mchana,

kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.

13 Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;

uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.

14 Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa

kwa namna ya ajabu na ya kutisha;

kazi zako ni za ajabu,

ninajua hayo kikamilifu.

15 Umbile langu halikufichika kwako,

nilipoumbwa mahali pa siri.

Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,

16 macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.

Siku zangu zote ulizonipangia

ziliandikwa katika kitabu chako

kabla haijakuwa hata moja.

17 Tazama jinsi yalivyo ya thamani

mawazo yako kwangu, Ee Mungu!

Jinsi jumla yake ilivyo kubwa!

18 Kama ningezihesabu, zingekuwa nyingi

kuliko mchanga:

niamkapo, bado niko pamoja nawe.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.